Audio & Video

Dkt. Emmanuel Gibai ahamasisha watanzania kutembelea hifadhi za Taifa

on

Watanzania wametakiwa kuendelea kuimarisha utamaduni wa kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa ikiwemo hgifadhi ya taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii hususani wanyama kupitia utalii wa ndani.

Mdau wa elimu nchini Tanzania, Dr.Emmanuel Gibai (wa kwanza kushoto) anayasema hayo Agosti 08, 2018 baada ya kutembelea hifadhi ya taifa Serengeti kupitia fursa iliyotolewa kwa watanzania na TANAPA kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Pia wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM kutoka wilaya ya Bunda mkoani Mara waliitumia fursa hiyo kutembelea hifadhi ya taifa Serengeti kama ambavyo baadhi yao wanaonekana katika picha akiwemo Katibu wa chama hicho wilaya (wa pili kulia).

“Watanzania tujenge utamaduni wa kutembela hifadhi zetu na kutambua fursa zilizopo kwenye utalii ikiwemo kutengeneza na kuuza bidhaa asilia na kujipatia kipato”. Alisisitiza Dkt. Gibai. 

 

Recommended for you