Audio & Video

Karibu kwenye Mkutano Mkubwa wa Injili “OYES 2018” Jijini Mwanza

on

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Dkt.Daniel Moses Kulola anakukaribisha kwenye mkutano mkubwa wa injili wa OYES (Open Your Eyes and See-Fungua Macho yako na Uone) 2018 kuanzia jumanne Februari 13,2018 hadi jumapili tarehe Februari 18,2018.

Mkutano huo utafanyika kwenye viunga vya kanisa hilo lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na tayari wahubiri kutoka Canada wamekwisha wasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kuhudumu kwenye mkutano huo.

Kutakuwa na huduma ya maombezi kwa watu wote bure ambapo pia kwaya mbalimbali zitahudumu kwenye mkutano huo utakaokuwa ukianza saa sita alasiri hadi saa 12 jioni.

Usikoseee!

Recommended for you