Habari Picha

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AWAASA WANAHABARI KUONGEZA KASI YA KUANDIKA HABARI ZINAZOHUSIANA NA UTALII HAPA NCHINI. ATOA HAMASA KWA WATANZANIA KUUKUZA UTALII WA NDANI.

on

Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Tarish Maimuna

Waandishi wa habari hapa nchini
wameaswa kuongeza kasi ya kuandika habari zinazohusiana na vivutio mbalimbali
vya Utalii, kwa lengo la kuongeza na kukuza uelewa juu ya umhimu wa Utalii
katika jamii, jambo litakalosaidia kukuza Utalii wa ndani na nje hapa nchini.

Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tarish Maimuna ameyasema hayo hii leo Mkoani
Mwanza, wakati akifungua Mkutano wa Siku Tatu ulioanza leo baina ya Shirika la
Hifadhi za Taifa nchini TANAPA na Wahariri wa Vyombo mbalimbali hapa nchini.

“Ili Utalii
uweze kukua, hususani Utalii wa ndani jamii ni lazima ipate taarifa sahii
Kuhusiana na Vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini, hivyo wanahabari na
Vyombo vya habari kwa ujumla wanapaswa kuongeza kasi katika kuandika habari
zinazohusiana na Utalii”.Alisema Maimuna.

Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Tarish Maimuna
Kuhusu
Utalii wa ndani hapa nchini, amesema kuwa bado hali siyo nzuri hivyo vyombo vya
habari viongeze hamasa ya kuhamasisha wanajamii kutembelea vivutio vilivyopo
hapa nchini huku akibainisha kwamba pamoja na umhimu wa Utalii wa nje, bado
utalii wa ndani unachangia katika utalii endelevu hapa nchini.

Aidha
amebainisha kuwa amebainisha kuwa Sekta ya Utalii ni miongoni mwa Setka
zinazochangia kwa asilimia kubwa katika uchumi wa Taifa sanjari na Kuongeza
upatikanaji wa ajira hapa nchini.

“Mwaka jana
pekee Sekta ya Utalii ililiingia Taifa Dolla za Kimarekani Bilioni 1.8 huku
ikitoa ajira za moja kwa moja na Zisizo za moja kwa moja zipatazo Milioni Moja,
Laki moja Tisini na Tisa elfu ambapo jumla ya Watalii wa nje Milioni Moja, Laki
moja thelathini na tano elfu Mia nane themanini na nne”, Alisema Maimuna huku
akiongeza kuwa Sekta ya Utalii ni sekta ambayo inaweza kumnufaisha kila mtu
katika jamii, mfano mama ntilie ambao hujiajiri katika maeneo ya Utalii.
Kaimu Katibu Tawala Mkoani Mwanza Cresencia Joseph
Azungumza
katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TAPANA, Ibrahim Mussa ambae ni
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko kutoka TANAPA, alibainisha kuwa Mikutano baina
ya TANAPA na wanahabari imekuwa ikiongeza tija katika Sekta ya Utalii hapa
nchini ambapo Mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka jana Mkoani Iringa na baada ya
Mkutano huo habari juu ya Utalii ziliongezeka hadi kufikia asilimia 92.

Aidha
alibainisha kuwa bado utalii wa ndani ni changamoto kubwa katika sekta ya
utalii hapa nchini kwa kuwa Watanzania wengi hawana desturi ya kutembea vivutio
vya utalii hapa nchini, ambapo ameahidi kuwa TANAPA itaendelea kutoa
ushirikiano wake ili kufanikisha utalii wa ndani hapa nchini badala ya
kutegemea Utalii wan je.

Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa
Wanahabari
Kwa Upande
wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Cresencia Joseph ambae amemwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Mkutano huo, alitoa rai kwa washiriki wa Mkutano
huo kutoka na maadhimio ya pamoja juua ya nini cha kufanya ili kupambana na
Ujangili katika hifadhi za Taifa hapa nchini.

Nao baadhi
ya Washiriki wa Mkutano huo ambao ni baadhi ya Wahariri kutoka vyombo
mbalimbali vya habari hapa nchini, waliozungumza nje ya Ukumbi wa Mkutano huo
wameeleza kuwa vyombo vya habari vina Mchango Mkubwa wa Kukuza Sekta ya Utalii
hapa nchi huku wakibainisha kuwa habari sahihi juu ya Utalii wa ndani bado
zinahitajika ili kukuza utalii huo kwa kuwa bado hakuna taarifa sahihi juu ya
utalii wa ndani katika jamii.

                                                 
Mkutano
huo unafanyika katika Ukumbi wa Hotel ya JB Belmont Jiji Mwanza umeanza leo
Jumatatu na unatarajiwa kutamatishwa Alhamisi ya may 29 wiki hii ambapo pamoja
na Mada nyingine, Mada kuu inayojadiliwa inaendana na Kaulimbiu ya mwaka huu
inayosema “Wajibu wa Vyombo vya habari katika kuuza Utalii”.