Habari Picha

KATIBU MWENEZI WA CCM AANGUKA GHAFLA JUKWAANI MKOANI SHINYANGA. USHIRIKINA WAHUSISHWA.

on

Na:Shaban Njia
KATIBU wa itikadi, Uenezi na siasa wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga Masoud Melimeli ameugua ghafla muda mfupi baada ya kushuka jukwaani alipokuwa akimnadi mmoja wa wagombea wa udiwani (CCM) na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya hiyo kwajili ya kupatiwa matibabu.
Tukio hilo ambalo lilihusishwa na imani za kishirikina lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni baada ya Melimeli kushuka jukwaani alipokuwa akimnadi mgombea Udiwani kata ya Kahama mjini Khamidu Juma Kapama.
Melimeli ambaye aliyekuwa akimnadi mgombea Udiwani huyo huku akitamka maneno makali ya kumshambulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama katika kipindi kilichopita James Lembeli aliyekihama chama cha Mapinduzi na kuhamia Chadema.
Muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgombea Udiwani huyo ili kuongea na wananchi wa Kata hiyo, Melimeli alijikuta akiishiwa nguvu na kuanguka jukwaani kabla ya kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Akizungumza kwa njia ya simu, Melimeli alisema kuwa ugonjwa unaomsubua haupaswi kutibiwa hospitalini hapo bali unatakiwa kutibiwa sehemu nyingine tofauti na hospitali na kwamba anapumzika sehemu ambayo hakuitaja.
“Kwa sasa nipo sehemu nimepumzika kwani ugonjwa huu siyo wakutibiwa hospitalini, hospitali nimekwenda kutibiwa na ugonjwa haujabainika hivyo unahitaji kutibiwa sehemu nyingine na siyo hapo wacha ni pumzike nitapona tu mungu yupo asanteni”. Alisema Melimeli.
Kabla ya kukumbwa na maswaibu hayo, Melimeli aliwasihi wananchi kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais kwa kuwa hao ndiyo wenye uwezo wa kuwatumikia kimaendeleo.

Recommended for you