Audio & Video

Kauli ya Makamu Mwenyekiti Mpya BAVICHA Bara baada ya kuwasili Mwanza

on

Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAVICHA lilikutana Jijini Dar es salaam Disemba Mosi mwaka huu na kuwachagua viongozi wake kufuatia aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Patrobas Katambi kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM hivi karibuni.

Baraza hilo lilimchagua aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Bavicha Bara, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti, Mwl.John Pambalu ambaye pia ni diwani wa Kata ya Butimba Jijini Mwanza kuwa Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanziba akiendelea kuwa Zeudi Mvano Abdullah ambapo viongozi hao watakaa madarakani kwa mwaka mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi hapo mwakani.

Kufuatia mabadiliko hayo, hii leo jumatano Disemba 06,2017 Mwl.Pambalu amezungumza na BMG baada ya kuwasili Jijini Mwanza…

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you