Habari Picha

Matukio mbalimbali kutoka Bujora Mwanza kwenye kilele cha tamasha la Bulabo

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Tulia Ackson leo Juni 10,2018 anafunga maadhimisho ya ngoma za kabila la Wasukuma maarufu kama tamasha la Bulabo katika uwanja wa Kisesa Magu mkoani Mwanza.

Mhe.Ackson akiambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amewasili katika Kituo cha Kuhifadhi na Kuendeleza Utamaduni wa kabila la Wasukuma Bujora na kujionea kumbukumbu mbalimbali kituoni hapo.

Tamasha la Bulabo lilifunguliwa jumapili iliyopita Juni 03,2018 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ambapo alipewa jina la kisukuma Masanyiwa alisema serikali itashiriki kuboresha kituo cha Bujora. Tazama HAPA ufunguzi.

Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson akisalimiana na Machifu wa Kisukuma alipowasili katika viwanja vya Bujora. Kilele cha ngoma za Bulabo kinafanyika katika uwanja wa mpira Kisesa

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mhe.Stanslaus Mabula (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa taasisi ya First Community ya Jijini Mwanza, Ahmed Misanga wakifurahia jambo walipokutana Bujora.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa pili kulia), akiteta jambo na viongozi mbalimbali alipowasili katika vounga vya Bujora

Mkurugenzi wa Kituo cha Bujora, Padri Fabian Mhoja (wa pili kulia), akitoa maelezo mbalimbali kuhusiana na kituo hicho kwa Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson

Recommended for you