Audio & Video

Waziri Mkuu awahimiza Wasabato kuendelea kushirikiana na serikali

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ametoa rai kwa Kanisa la Waadventista Wasabato kuendelea kuiunga mkono serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kuwawezesha waumini wake kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza jana kwa niaba ya Mhe.Majaliwa kwenye mkutano wa Ufunuo wa Matumaini ulioandaliwa na kanisa hilo Jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alisema kanisa lina fursa ya kuwawezesha waumini wake kuunda vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali na kuvisaidia kupata mitaji.

Aidha alilipongeza kanisa hilo kwa kuungana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwepo kutatua changamoto za maji kwa kuchimba visima, ujenzi wa shule, vyuo, vituo vya afya pamoja na hospitali.

Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kanda ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Marekana alisema kanisa litaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rasi Dkt.John Pombe Magufuli.

Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini ulianza Mei 12, 2018 hadi Juni 02, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo mhubiri mkuu alikuwa Mchungaji Mark Finley kutoka nchini Marekani.

Viongozi wa kamati waliofanikisha mkutano wa Ufunuo wa Matumaini Jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto), akiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ambapo alimwakilisha Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Mkutano wa Injili wa Ufunuo wa Matumaini ulioandaliwa na Kanisala la Waadventista Wasabato. 

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto), akiambata pamoja na Mchungaji Godwin Lekundayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu ka Kaskazini.

Mchungaji Godwin Lekundayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu ka Kaskazini akizungumza kwenye kilele cha Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini uliofanyika CCM Kirumba Jijini Mwanza, tangu Mei 12, 2018 hadi Juni 02, 2018. 

Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kanda ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Marekana (kushoto), akimtambulisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia) aliyemwakilisha Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.

Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kanda ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Marekana (kushoto), akimtambulisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia) aliyemwakilisha Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.

Baadhi ya viongozi wa kamati waliofanikisha mkutano huo.

Viongozi wa kamati waliofanikisha mkutano huo.

Maelfu ya wananchi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato walihudhuria mkutano huo.

Zaidi ya waumini 2000 walibatizwa kwenye mkutano huo Jijini Mwanza.

Muhubiri Mkuu kwenye mkutano huo alikuwa Mchungaji Mark Finley kutoka nchini Marekani.

Ndani na nje ya Tanzania, takribani waumini elfu 20 walibatikwa baada ya kufuatilia mubashara mkutano huo kwa njia mbalimbali ikiwemo ikiwemo runinga, redio pamoja na mitandao ya kijamii.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), akiteta jambo na Mchungaji Mark Finely (kulia) kutoka Marekani. Katikati ni mke wa mchungaji Finley, Ereneste Finley.

 

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Waziri Nchemba afungua Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini

Recommended for you