Michezo

KIPIGO CHA MAGOLI CHATAWALA MICHUANO YA NDONDO CUP JIJINI MWANZA

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Timu ya Power Fc ya wilayani Ilemela imeilaza vibaya timu ya  Nyakato Steel kwa goli  4 -3, katika mashindano ya Ndondo cup yanayoendelea kutimua vumbi kwenye uwanja wa Nyamagana jijini hapa.
Mchezo huo ambao ni wa raundi ya pili hatua ya makundi ulizikutanisha timu zote kutoka kundi C.

Mabao ya Power FC yalifungwa na Mohamed Kitambi dk ya 23, Deogratias Nyalinga dk 43, Slum Kabunda dk 54 na Haji Burhani dk ya 66. Nyakato steel walipata mabao yaokupitia Faida Edward dk ya 14, Hamad Sudi dkya 51 na Rajab Henrico dk ya 77.

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Power FC, Maganga Seif ameipongeza timu yake kwaushindi huo,pia alisema ana imani kubwa na timu yakehivyo itaedelea kupambana ili kuhakikisha inasonga mbele na kufuzu katika hatua inayofuata.

Golikipa huyo wa zamani wa Toto Africans na Geita gold sc alisema timu yake ilicheza vyema licha ya kushindwa kutumia nafasi ilizotengeneza katika vipindi vyote.

Kocha mkuu wa timu ya Nyakato steel, Emily Yusuph alisema amekubali kipigo hicho na ameahidi timu yake itacheza kumalizia ratiba dhidi ya Bwiru stars.

Katika mchezo mwingine timu ya AFC Lumumba iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bwiru stars. Mabao ya AFC Lumumba yalifungwa na Boniphace Mutaleba katika dk ya 49, 53 na 59 huku mabao ya Bwiru stars yakifungwa na Radius Malugu dk ya 26 na Kibo Marti.

Recommended for you