Audio & Video

Kituo cha Uwekezaji Tanzania chajidhatiti kuwasaidia wawekezaji

on

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa, Fanuel Lukwaro (kulia) akisalimiana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage na kupokea kikombe na cheti baada ya kuibuka mshindi kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika viunga vya Rock City Mall.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimewahimiza watanzania kutumia vyema fursa inayotolewa na kituo hicho ya kuwasaidia kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji hususani kwenye sekta ya viwanda.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa, Fanuel Lukwaro wakati akizungumza na wanahabari kwenye maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza yanayoandaliwa na TCCIA.

Alisema kituo hicho kimejidhatiti kuwasaidia wawekezaji ambapo kinafuatilia vyema kwa ukaribu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuwasaidia kutimiza taratibu zote za uwekezaji hususani katika sekta ya viwanda ambapo kituo hicho kupitia huduma za mahala pamoja huwasaidia wawekezaji kupata vibali vyote bila usumbufu.

Awali Afisa Habari TIC, Lafita Kigoma aliwahimiza watanzania kufika kwenye banda la kituo hicho ili kupata ushauri kuhusiana na namna bora ya uwekezaji ambapo alibainisha hivi sasa watanzania wanahamasishwa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda vya kutengena dawa za binadamu na vifaa tiba, mafuta ya kula, viwanda vya kuongeza thamani kwenye madini pamoja na kuongeza thamani mazao ya kilimo lengo likiwa ni kuifikia Tanzania ya viwanda ifika mwaka 2025.

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa, Fanuel Lukwaro akifurahia ushindi wa taasisi hiyo kwa kuonesha kombe na cheti

Baadhi ya viongozi, washiriki na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa maonesho hayo

Mgeni rasmi Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage (waliokaa katikati), Mkurugenzi wa Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini TANTRADE, Edwin Rutageruka (kushoto waliokaa) pamoja na Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari (kulia waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa jumla waliojiandaa vyema kushiriki maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki ambao ni kampuni ya TLED

Tazama BMG Online Tv hapa chini

Recommended for you