Audio & Video

Kivuko kipya na cha kisasa MV.Mwanza chashushwa rasmi Ziwa Victoria

on

Mwonekano wa kivuko kipya cha MV.Mwanza kabla ya kushushwa majini. Ujenzi ulianza Oktoba mwaka jana chini ya kampuni ya Songoro Marine Transport, katika fukwe zilizopo eneo la Tunza Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kivuko kipya na cha kisasa cha MV.Mwanza kimeshushwa rasmi hii leo katika maji ya Ziwa Victoria kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za ukarabati kabla ya kuanza kufanya kazi.

Viongozi na wananchi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella, wameshuhudia tukio hilo na kutoa pongezi kwa serikali na kampuni ya Songoro Marine Transport kwa ujenzi wa kivuko hicho.

“Hatujamaliza hata miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini vitu vinavyofanyika utadhani tuna miaka 10 tayari na kwa jinsi Mhe.Rais anavyotupeleka tutakuwa mbali sana baada ya miaka 10”. Amesema Mhe.Mongella.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Songoro Marine Transport, Saleh Songoro amesema kivuko hicho kitakuwa tayari kufanya kazi baada ya wiki tatu baada ya kushushwa majini.

Kivuko cha MV.Mwanza kimegharimu shilingi bilioni 8.9 na kina uwezo wa kubeba tani 250 ambazo ni sawa na magari 36 na abiria 1000 ambapo wananchi wamefurahishwa na ujio wa kivutko hicho wakisema kitasaidia kurahisha huduma za usafiri katika eneo la Kigongo-Busisi kwa kushirikiana na kile cha MV.Misungwi chenye uwezo pia wa kubeba tani 250.

Mwonekano wa kivuko cha MV.Mwanza baada ya kushushwa majini, Ziwa Victoria

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza baada ya MV.Mwanza kushushwa majini

Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa tatu kulia) wakishuhudia kivuko cha MV.Mwanza kikishushwa majini. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya Magu na Kaimu Mkuu wa Wilaya Ilemela Mhe.Khadija Nyembo na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Songoro Marine Transport, Saleh Songoro

SOMA MV.Nyehunge kurahisisha usafiri wa Mwanza-Ukerewe

Recommended for you