Audio & Video

Kiwanda cha chupa Mkuranga mkoani Pwani

on

Kampuni ya Kioo Ldt inayochimba mchanga wa madini ya kutengeneza chupa katika Kijiji cha Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, imeahidi kushiriki vyema katika miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia fedha za huduma za jamii wilayani humo.

Afisa Msimamizi wa kampuni hiyo, Richard Kisyombe anaeleza hayo mbele ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko aliyefanya ziara katika machimbo hayo Oktoba 23, 2018.

Biteko pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza chupa cha kampuni hiyo na kuutaka uongozi wake kuandaa mpango kazi wa namna itakavyoshiriki shughuli za maendeleo.

Tazama BMG Online TV hapa chini.

SOMA>>>Biteko awataka wawekezaji kuandaa mipango ya kuhudumia wanajamii

Recommended for you