Michezo

Kocha Pamba atangaza kiama michezo iliyosalia Ligi Daraja la Kwanza 2017

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Kocha msaidizi wa timu ya Pamba SC, Salmin Kamau amesema atafanyia kazi safu ya washambuliaji ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yake iliyobaki.

Aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika  kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza unaoendelea nchini uliozikutanisha timu ya Pamba SC  na JKT Oljoro,uliotimua vumbi kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Katika mchezo huo Pamba SC ilitoa kichapo cha goli 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kupitia Peter Magata dakika ya 38, hivyo kufatia ushindi huo timu hiyo inakua na jumla ya point 12.

Kamau alisema katika mchezo huo ameona madhaifu ya washambuliaji kutokuwa makini,hivyo atalifanyia kazi ili kuhakikisha mechi zilizosalia wanafanya vizuri na kushinda sambamba na kuongeza safu ya washambuliaji.

Kwenye mchezaji huo, mchezaji wa Pamba SC Juma Nyangi alikuwa kivutio  katika mchezo huo, baada ya timu yake kushinda rufaa dhidi ya Alliance FC waliokua wamemkatia rufaa wakidai ni  mchezaji wao.

Mchezaji huyo akimshukuru Mungu kurejea tena uwanjani pamoja na timu yake kuibuka na ushindi huo.

Pia alisema, alikua anaumia pale timu yake ilivyokuwa ikifungwa hivyo aliwaahidi mashabiki wake kutegemea ushindi katika mechi zilizosalia.

Recommended for you