Audio & Video

Walichopanga kufanya wahandisi baada ya kukutana Jijini Mwanza

on

Judith Ferdinand, BMG

Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini imeweka mikakati ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na wahandishi wazawa wenye uwezo wa kubuni na kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo magari pamoja na simu.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Mhandisi Patrick Barozi alitoa kauli hiyo jana kwenye kongamano lililofanyika Rock City Mall katika kuelekea Septemba 05, 2018 ikiwa ni kilele cha kusherekea miaka 50 ya bodi hiyo.

Alisemani vyema kuwahimiza wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kuendelea kupata wataalamu vijana ambao watakuwa wabunifu ili wasaidie kufikiwa lengo hilo huku serikali ikiendelea kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kupata ujuzi wa kutosha.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Mtemi Msafiri ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Kwimba aliwahimiza washiriki wa kongamano hilo kujadili namna bora ya kufikia Tanzania ya Viwanda na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono wakandarasi wazawa.

PIA SOMABenki ya CRDB yawahakikishia dhamana ya kazi na mikopo Wakandarasi 

Recommended for you