Habari Picha

VIWANDA: Mwakilishi Mkazi wa UN ataka vyombo vya habari vishirikishwe

on

Judith Ferdinand, BMG

Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili Taifa lifikie uchumi endelevu wa viwanda, ni vyema serikali ikavishirikisha ipasavyo vyombo vya habari.

Rodriguez aliyasema hayo jana Jijini Mwanza kwenye kongamano maalum la kitaaluma lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino SAUT na kuongeza kwamba vyombo vya habari vinapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko ya watunga sera kuelekea Tanzania ya viwanda.

Alisema vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwani ni njia sahihi ya wananchi na serikali kupaza sauti namna bora ya kufikia uchumi wa viwanda hivyo ni vyema serikali ikavipa kipaumbele ili kufanikisha azima hiyo.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha SAUT, Dotto Bulendu alisema kongamano hilo limeandaliwa na chuo hicho kitivo cha habari za uchunguzi katika eneo la biashara pamoja na sera kupitia udhamini wa shirika la Best Dialogue lengo. Alisema ili ajenda ya uchumi wa viwanda ieleweke vyema, vyombo vya habari lazima vitumike ipasavyo kutoa elimu kuhusiana na sekta ya viwanda huku akiwahimiza wanahabari kutambua vyema sera za nchi kuhusiana na mazingira ya biashara.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo walisema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi na wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya viwanda na hivyo kufikia lengo lililokusudiwa na Tanzania ya viwanga kama ilivyo azima ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza kwenye kongamano maalum la kitaaluma lililofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Jijini Mwanza. Kongamano hilo lilibatizwa jina la aliyekuwa Mhadhiri  wa chuo hicho marehemu Nkwabi Ng’wanakilala.

Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT, Dotto Bulendu akionyesha kitabu kilichoandikwa na aliyekuwa Mhadhiri wa chuo hicho marehemu Nkwabi Ng’wanakilala kwenye kongamono hilo

Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha SAUT, Dotto Bullendu akionyesha kitabui kilichoandikwa na aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo hicho marehemu Nkwabi Ng’wanakilala

Mkurugenzi wa shirika la utangazaji Tanzania TBC, Dkt.Ayub Rioba akizingumza na wanahabari kadno ya kongamano hilo

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo

Kongamano maalum la kitaaluma lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT kampasi kuu ya Malimbe Jijini Mwanza

Recommended for you