Habari Picha

KUHUSU BASI LA BATCO KUWAKA MOTO MKOANI MARA.

on

Basi la kampuni ya Batco lenye namba za usajili T.192 DHW leo limeteketea kwa moto katika eneo la Kirumi Kata ya Bukabwa Wilayan ya Butama mkoani Mara.
Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza ambapo chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zilizoteketea kwa moto na hakuna mtu aliyepoteza maisha.