Michezo

KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA TFF ULIOFANYIKA MKOANI DODOMA

on

 Wallace Karia (kulia) akiapishwa na Mwanasheria wa BMT, kuwa Rais mpya wa TFF mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma. Katika uchaguzi huo Karia aliibuka na jumla ya kura 95 akiwambwaga wapinzani wake Ally Mayay, na Richard Shija waliopata kura tisa kila mmoja, Iman Madega kura nane, Frederick Mwakalebela kura tatu na Emmanuel Kimbe kura moja.

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzani TFF, yametangazwa jioni hii Mjini Dodoma baada ya zoezi la upigaji na uhesabuji wa kura kukamilika.

Wallance Karia amechaguliwa kuwa Rais wa TFF katika uchaguzi huo kwa kura 95 kati ya wajumbe 128 waliopiga kura. Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emmanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi hiyo ya uras.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa Makamu wa Rais chini ya Rais Jamal Malinzi ambapo baadaye aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuswekwa mahabusu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi. Karia ataiongoza TFF kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo.

Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TFF ni; Zone 1 Saloum Chama, Zone 2 Vedastus Lufano, Zone 3, Mbasha Matutu, Zone 4 Sarah Chao, Zone 5 Issa Bukuku, Zone 6 Kenneth Pesambili, Zone 7 Elias Mwanjala, Zone 8 James Mhagama, Zone 9 Dunstan Mkundi, Zone 10 Mohamed Aden, Zone 11 Francis Ndulane, Zone 12 Khalid Abdallah na Zone 13 ni Lameck Nyambaya.

Michael Wambura (kulia) akiapishwa na Mwanasheria wa BMT, kuwa Rais mpya wa TFF mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma.

Rais mpya wa TFF Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura, wakipongezana baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo.

Rais Wallace Karia akipongezwa na baadhi ya wajumbe.

Michael Wambura akipongezwa na mmoja kati ya wajumbe

Karia akipongezwa

Baadhi ya wagombea walioangukia pua katika uchaguzi huo, kutoka (kushoto) Emmanuel Kimbe, Iman Madega, Richard Shija, Frederick Mwakalebela na Mtemi Ramadhan,wakijadili jambo baada ya kupiga kura na kupata tetesi ya matokeo. Picha na Sufian Mafoto

 

 

Recommended for you