Audio & Video

Mkuu wa mkoa Mwanza aja na mkakati kabambe kwa wanafunzi

on

George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amekuja na mkakati ambao kama utatekelezwa vyema utasaidia kupunguza utoro mashuleni, kuongeza ari ya kusoma na hatimaye kuongeza idadi ya ufaulu.

Mhe.Mongella alikuwa akizungumza hii leo Mei 14, 2018 kwenye kikao kazi cha waalimu wakuu, maafisa elimu kata, wilaya, ofisi ya mkuu wa mkoa na wadhibiti ubora kutoka halmashauri zote nane za mkoa wa Mwanza ambazo ni Nyamagana, Ilemela, Magu, Ukerewe, Buchosa, Sengerema, Misungwi pamoja na Kwimba.

Halmashauri ya Misungwi yapiga hatua sekta ya elimu

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye kikao hicho.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza RC Mongella.

Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Elimu mkoani Mwanza, Mwl. Michael Ligola akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Elimu Msingi halmashauri ya wilaya ya Kwimba, Emmanuel Johnson akitoa maoni yake kuhusiana na mkakati wa wanafunzi mkoani Mwanza kupewa chakula cha mchana.

Recommended for you