Audio & Video

Maabara ya Kisasa ya TFDA Kanda ya Ziwa kuleta ahueni kwa Wananchi

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Wafanyabiashara wakiwemo wazalishaji wa bidhaa mbalimbali Kanda ya Ziwa, wametakiwa kuitumia vyema Maabara ya Kisasa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA iliyopo Jijiji Mwanza ili kufanya uchunguzi wa bidhaa zao kabla ya kuziingiza sokoni.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya aliyasema hayo jana baada ya kufanya ziara ya kukagua ufungwaji wa mashine za maabara hiyo, kujionea utendaji pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TFDA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Agnes Kijo alisema uwepo wa maabadara ya hiyo Kanda ya Ziwa, utasaidia uchunguzi wa bidhaa mbalimbali kukamilika kwa wakati na hivyo kuwaondolea usumbufu wazalishaji wa bidhaa hizo wakiwemo wenye viwanda vidogo vidogo.

Serikali kwa kushirikiana na taasisi ya Global Fund imefanikisha upatikanaji wa mashine za kisasa katika ofisi za TFDA Kanda ya Ziwa pamoja na Makao Makuu vilivyogharimu zaidi ya shilingi bilioni tano.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya, amefanya ziara katika Maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Ziwa kujionea ufungwaji wa vifaa katika maabara hiyo pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya, akikagua maabara ya kisasa ya TFDA Kanda ya Ziwa.

Maabara hii itasaidia kwenye uchunguzi wa sampuli mbalimbali hususani kwa wazalishaji wadogo wa chakula na dawa.

Maabara hii inafungwa vifaa vya kisasa vitakavyowezesha uchunguzi kufanyika kwa haraka na kwa uhakika zaidi.

Maabara hii ni mkombozi kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali Kanda ya Ziwa wakiwemo wenye viwanda vidogo vidogo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya (kulia) akizungumza na wanahabari baada ya kufanya ukaguzi wa maabara ya TFDA Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFDA, Agnes Kijo.

Afisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Ziwa, akifafanua jambo kwa wanahabari baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya kufanya ziara katika maabara ya mamlaka hiyo.

Recommended for you