Audio & Video

Wanafunzi nao waguswa na suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

on

BMG Habari-Pamoja Daima

Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa taifa moja la Tanzania Aprili 26, 1964 ikiwa ni ushirikiano baina ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume pamoja na aliyekuwa Rais wa Tanganyika Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Wawili hao walitia saini mkataba wa makubaliano Aprili 22, 1964 na kuthibitishwa na bunge na Tanganyika pamoja na Baraza la Mapinduzi Zanzibar Aprii 26, 2964 ambapo Aprili 27 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kibadilishana hati za muungano.

Sheria za Muungano ilitamka kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61 ya mwaka 1964.

Msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.

Hivyo basi Aprili 26 ya kila mwaka watanzania huungana pamoja kusherehekea muungano wa Tanganyika na Tanziabr ambapo mwaka huu 2018 ni Maadhimisho ya 54 na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameongoza maadhimisho hayo kitaifa mjini Dodoma.

Bonyeza kwa habari zaodi

Recommended for you