Audio & Video

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza afungua Maadhimisho ya Wiki ya Bandari

on

George Binagi-GB Pazzo @BMG Habari

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amefungua Maadhimisho ya Wiki ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA mkoani Mwanza, yanayoadhimishwa mwaka huu ikiwa ni miaka 13 tangu kuanzishwa mamlaka hiyo.

Mongella alifungua maadhimisho hayo jana Aprili 10,2018 na yatafikia tamati Aprili 15, 2018 katika viunga vya Bandari ya Mwanza Kaskazini na kuipongeza TPA kwa kazi kubwa na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Daniel Sira alisema TPA ilianzishwa Aprili 14, 2005 kupitia sheria ya bandari nambari 17 ya mwaka 2004 na ilianza kufanya kazi rasmi Aprili 15, 2005 kwa kupewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza bandari zote nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Bandari mkoani Mwanza.

Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Daniel Sira akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akipokea taarifa kwenye mabanda yaliyo katika maadhimisho hayo.

 

 

Recommended for you