Habari Picha

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAIPONGEZA TAASISI YA ADLG

on

Taasisi ya kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini ADLG leo imewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka mikoa ya Shinyanga na Geita kwa ajili ya kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali kuhusiana na raslimali madini.
Ni kupitia mijadala ya asubuhi “Breakfast Dialogue” inayofanyika mara kwa mara ambayo hufanywa na taasisi hiyo ambapo pia wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari hushiriki.
Mjadala wa hii leo umefanyika Jijini Mwanza na kuwahusisha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka halmashauri za Msalala, Kahama, Geita na Bukombe ambapo maafisa hao wameipongeza taasisi ya ADLG kwa kuwajengea uwezo wananchi wanaoishi katika maeneo yenye raslimali madini na kuahidi ushirikiano na taasisi hiyo.

Mratibu wa taasisi ya ADLG, Esther Masawe akizungumza kwenye mjadala wa hii leo
Mjumbe wa bodi ya ADLG, George Ramadhani akiwasilisha mada kwenye mjadala wa hii leo
Mwanahabari Gloria Kiwia akitoa uzoefu wake wa kazi katika maeneo yenye madini
Washiriki
Mwanahabari Clara Matimo akitoa uzoefu wake wa kazi katika maeneo yenye madini

Recommended for you