Audio & Video

SEKTA YA AFYA- Serikali yapongezwa wilayani Misungwi

on

Zahanati ya Kijiji cha Ngeleka Kata ya Fela wilayani Misungwi iliyojengwa.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imeipongeza serikali kwa jitihada kubwa za kuboresha huduma za afya wilayani humo ikiwemo ujenzi wa jengo upasuaji (wodi ya mama na mtoto) katika Kituo cha Afya Kata ya Mbarika.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Misungwi, Daud Gambadu alitoa pongezi hizo juzi baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/20.

“Naipongeza serikali yetu kwa kubuni na kuanzisha mradi huu, naamini ni mradi ambao utatuokoa wanawake kwa kutoa huduma nzuri kwani Vijiji ama Kata zilizoko huku ziko mbali sana hivyo kumtoa mgonjwa kumpeleka hospitali ya wilaya inanawezana kabisa akapatwa na madhara makubwa njiani, lakini kutokana na mradi huu wanawake watapata huduma iliyo karibu”. Alipongeza Katibu wa CCM wilayani Misungwi, Latifa Malimi.

Mganga Mkuu wilayani Misungwi, Dr.Zabron Masatu alisema ujenzi wa chumba cha upasuaji pamoja na wodi ya kupumzikia wagonjwa baada ya upasuaji katika Kituo cha Afya Mbarika unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wadau kupitia mradi wa Mama na Mtoto kwa gharama ya shilingi Milioni 203 na ukilenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Tarafa ya Mbarika pamoja na maeneo jirani.

Jengo kama hilo (wodi ya mama na mtoto) pia linajengwa katika Kituo cha Afya Misasi kwa ushirikiano baina ya serikali, ubalozi wa Ireland, nguvu za wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Jengo la Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Mbarika wilayani Misungwi.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Misungwi Daud Gambadu (kushoto), akimsikiliza Mganga Mkuu wilayani humo Dr.Zabron Masatu wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Misasi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya Misungwi Juma Sweda (katikati) pia walijumuika kwenye ziara hiyo.

Bonyeza BMG ziara Kamati ya Siasa ama bonyeza BMG Habari maboresho ya Kituo cha Afya Karume.

Recommended for you