Audio & Video

Biteko awaonya wasio na vifaa kinga machimbo ya jasi wilayani Same

on

Naibu Waziri wa Madini Mwl. Doto Mashaka Biteko (kulia) akizungumza na baadhi ya wachimbaji wa madini ya viwandani aina ya jasi (Gypsum) ya Chakoko yaliyopo katika Kijiji cha Makanya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mwl. Biteko alifanya ziara ya kutembelea machimbo hayo na baadae kuzungumza na wachimbaji na wamiliki wa leseni za madini ambapo aliwataka wamiliki wote wa leseni katika machimbo hayo kuhakikisha wanazingatia usalama mahala pa kazi kwa kuwapa wafanyakazi vifaa kinga ikiwemo kofia ngumu pamoja na vikinga vumbi.

Alimwagiza Afisa Madini mkoani Kilimanjaro, Fatma Kyando kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa ndani ya wiki tatu na kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Mmoja wa wachimbaji madini ya jasi aliyekutwa hana vifaa kinga katika machimbo ya Chakoko wilayani Same.

SOMA>>>Wamiliki wa leseni Mererani watakiwa kulipa madeni yao

Recommended for you