Audio & Video

Wachimbaji mchanga Mkuranga wahofia ajira zao kutoweka

on

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akiwasikiliza wachimbaji wa mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani alipofanya ziara katika machimbo hayo kujionea uendeshaji wa shughuli na ulipaji kodi stahiki za serikali.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wamiliki wa leseni ya uchimbaji mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilayani Mkuranga na kukagua vitabu vya ripoti za uendeshaji wa shughuli zake.


Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wachimbaji wa mchanga katika machimbo ya Mwanadilatu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, wamelalamikia ujio wa mashine za “skaveta” (Excavator) katika machimbo hayo kwa hofu ya kupoteza nafasi zao za kazi.

Katibu wa wachimbaji hao, Seleman Zombe anasema hatua hiyo itaathiri wachimbaji wengi wakiwemo vijana wanaokadiriwa kufikia 1,000 na hivyo kuomba serikali kuzuia mashine hizo kufanya kazi katika machimbo hayo.

Hayo yamejiri Oktoba 23, 2018 baada ya Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kufanya ziara katika machimbo hayo kukagua uendeshaji wa shughuli za uchimbaji mchanga na ulipaji wa kodi stahiki za serikali.

Hata hivyo Biteko alishtushwa na madai ya wachimbaji hao na kuwahimiza kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ambayo inarahisisha utendaji kazi ambapo alishauri wawekezaji wenye leseni katika machimbo hayo kuweka mikakati bora ya vijana hao kuendelea kufanya shughuli zao licha ya uwepo ya mashine za “skaveta”.

SOMA>>>Biteko aonya ukwepaji kodi katika machimbo ya Kaolin wilayani Kisarawe

Recommended for you