Audio & Video

RC John Mongella aingilia kati sakata la madai ya waalimu

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Inaelezwa kwamba zaidi ya waalimu 400 katika halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), wanadai madai mbalimbali ikiwemo uhamisho ambapo hii leo Mei 11, 2018 wamefika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella kuwasilisha malalamiko yao.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na baadhi ya waalimu Jijini Mwanza wanaodai madai mbalimbali ikiwemo ya uhamisho.

Mhe.Mongella ameahidi kukutana na waalimu hao baada ya wiki mbili.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba akifafanua jambo kwenye kikao hicho.

Afisa Tawala ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Baraka Nyamsendeka akifafanua kuhusu kanuni za utumishi wa umma katika kikao hicho.

Mmoja wa waalimu hao akiwasilisha malalamiko yake kwa niaba ya waalimu wengine.

Miongoni mwa madai ya waalimu hao ni pamoja na posho za uhamisho.

Waalimu hao wanalalamika baadhi ya waliohamishwa kulipwa stahiki zao huku wengine wakiachwa.

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (katikati), Mkuu wa wilaya Nyamagana Marry Tesha (kushoto), Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza Mhandisi Warioba Sanya (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye kikao hicho.

Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba (kushoto), wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza. 

Bonyeza BMG RC Mongella akipokea vitabu

Recommended for you