Habari Picha

Wananchi wilayani Misungwi wanufaika na mpango wa TASAF

on

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaitekele anasema mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini TASAF awamu ya tatu (TASAF III) ulianza kutekelezwa katika Halmashauri hiyo mwaka 2015/16 ambapo Vijiji 60 vyenye Kaya 8,985 vilianza kunufaika, mwaka 2016/17 Kaya 8,658 na mwaka 2017/18 kukiwa na Kaya 8,597 zinaendelea kunufaika na mpango huo.

Mwaitekele anasema maisha ya walengwa yamebadilika kiuchumi na mwitikio wa watoto kupata elimu na huduma bora za afya umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika halmashauri hiyo ambapo baadhi ya watoto hapo awali walikuwa hawawezi kuhudhuria shule kwa kukosa mahitaji kama mavazi pamoja akina mama wajawazito na watoto kushindwa kuhudhuria Kliniki.

Bi.Odilia Edward mkazi wa Kijiji cha Maswa wilayani Misungwi akipeleka mifugo aina ya mbuzi malishoni. Mifugo hii ilinunuliwa kupitia fedha za ruzuku kutoka TASAF awamu ya tatu

Bi.Felista Sabini mkazi wa Nyang’homango wilayani Misungwi akiwa na mifugo yake aliyoinunua kupitia ruzuku kutoka TASAF III

Bwana Idrisa Hassan ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Ntende wilayani Misungwi akiwa kwenye banda lake la mradi wa ufugaji kuku aliouanzisha baada ya kuanza kunufaika na ruzuku kutoka TASAF. Bwana Hassan ambaye ni mlemavu wa miguu sasa anamudu kuhudumia familia yake yenye watoto watoto na mke mmoja kupitia mradi huo

Kutokana na changamoto ya wezi, bwana Hassan ameuzwa kuku zaidi ya 150 na kuanza ujenzi wa nyumba yenye chumba kimoja, sebure, jiko na choo ili aweke moangaji na kujiongezea kipato na amebaki na kuku wachache wa mayai ambapo hukusanya trei mbili kwa wiki na kuziuza 24,000

Kupitia ruzuku kutoka TASAF, Bwana Hassan amejenga tenki la kuvuna maji ya mvua lenye ujazo wa mapipa 80

Bi.Ngollo Kilulu (wa pili kulia) mkazi wa Kijiji cha Misungwi na familia yake akiwa kwenye nyumba aliyoijenga baada ya kuanza kunufaika na ruzuku kutoka TASAF III

TASAF III pia imesaidia ujenzi wa visima 11 katika Kijiji cha Kimwa wilayani Misungwi na sasa wananchi wanafurahia huduma ya upatikanaji karibu maji safi

Wafugaji pia katika Kijiji cha Inonelwa Kata ya Misasi wanafurahia uwepo wa Lambo lililojengwa kwa ufadhili wa TASAF III kwa zaidi ya shilingi Milioni tisa

TASAF pia imesaidia upandaji miti kama shamba hili linavyoonekana katika Kijiji cha Kwimwa wilayani Misungwi

Wanafunzo ambayo Kaya zao zinanufaika na mpango wa TASAF sasa wanahudhuria vyema masomo na ufaulu unapanda

Mwitikio wa akina mama kuhudhuria Kliniki pia umeongezeka kutokana na hamasa kutoka mpango wa TASAF ambapo kuna malipo ruzuku maalum kwa akina mama wanaohudhuria Kliniki. Wananchi Halmashauri ya Misungwi sasa wanafurahia maisha kupitia mpango wa TASAF na wanaendelea kubuni na kuendeleza vyanzo mbalimbali vya uzalishaji mali ikiwemo ufugaji kuku ili kukuza kipato na uchumi wa Kaya.

Recommended for you