Audio & Video

Shirika la WoteSawa lawajengea Uwezo Maafisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Baada ya mafunzo haya, matumaini ni kuona washiriki hawa wanasaidia katika utetezi wa haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani ili kupunguza ukatili, unyonyaji na unyanyasaji kwa watoto hao.

Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WoteSawa, limetakiwa kutanua wigo wake na kuzifikia wilaya zote za mkoa wa Mwanza ili kusambaza elimu ya kupambana na ukatili katika jamii.

Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Wambura Kizito alitoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza, yaliyoandaliwa na shirika la WoteSawa.

Mratibu wa Shirika la WoteSawa Elisha Daudi, alisema shirika hilo kwa ufadhili wa Novo Foundation linatekeleza mradi wa miaka mitatu wa Uwezeshaji Shirikishi kwa Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani, ukilenga kuwajengea uwezo ili wajisimamie katika kupinga aina zote za ukatili na unyonyaji dhidi yao.

Aidha mradi huu pia unalenga kuwajengea uelewa wanajamii wakiwemo wazazi na waajiri kuhusu haki za watoto hususani haki ya kupata elimu kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani, kutoa msaada wa kisheria na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wahanga wa ukatili wa kazi za nyumbani.

Baada ya mafunzo haya, matumaini ni kuona washiriki hawa wanasaidia katika utetezi wa haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani ili kupunguza ukatili, unyonyaji na unyanyasaji kwa watoto hao.

Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Wambura Kizito akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa Miradi kutoka shirika la WoteSawa, Cecilia Nyangasi (kulia) pamoja na Joseph Mukoji (kushoto) ambaye ni mwanasheria wa shirika hilo wakifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Afisa Miradi kutoka shirika la WoteSawa, Cecilia Nyangasi.

Mratibu wa Shirika la WoteSawa Elisha Daudi, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani kwa kipindi cha mwaka jana.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa umakini taarifa hiyo.

Mwanasheria kutoka shirika la WoteSawa, Joseph Mukoji akiwasilisha mada kuhusu sheria zinazomlinda mtoto kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza ambazo ni Nyamagana, Ilemela, Magu, Misungwi, Sengerema, Kwimba na Ukerewe.

Bonyeza HAPA kutazama Mafunzo ya Afya ya Uzazi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza.

Recommended for you