Burudani

Mahafali ya kwanza ya Wafanyakazi wa Nyumbani Jijini Mwanza yafana

on

Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA lenye makazi yake Jijini Mwanza, limewawezesha wafanyakazi 17 wa nyumbani kupata mafunzo ya saluni katika chuo cha Friends Saloon.

Hii leo jumatano Machi 07,2018 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Merry Tesha amekuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Mahafali ya wanafunzi hao iliyofanyika ofisi za WOTESAWA zilizopo Capripoitn Jijini Mwanza.

“Mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani, yanaanza na mimi na wewe, Tuwawezeshe”- WOTESAWA.

Mhe.Tesha amesisitiza wanajamii kuungana pamoja kuhakikisha hakuna ukatili wa aina yoyote kwa wafanyakazi wa nyumbani. Fuatilia picha za mahafali hayo.

Recommended for you