Habari Picha

MAHAKAMA KUU KENYA YAREJESHA HESHIMA YA MAHAKAMA ZA AFRIKA

on

Mahakama Kuu nchini Kenya imetengua ushindi wa Rais wa sasa nchini humo, Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Raila Odinga na kwamba uchaguzi unapaswa kurudiwa ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.

Hatua hiyo imejiri kufuatia maombi ya mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake Raila Odinga ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, uliompa ushindi Rais Kenyatta.

Odinga alisema kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini PIA kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A, B na C hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matokeo.

 

Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6) wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya.

Ingwa  Mahakama hiyo imesema hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliobaini kwamba Rais Uhuru Kenyatta alitenda makosa katika mchakato wa uchaguzi huo wa Kenya uliofanyika Oktoba 08,2017.

Ulinzi ulikuwa umeimarisha nje ya Mahakama Kuu nchini Kenya. BMG kwa msaada wa Mitandao na Citizen Tv

Recommended for you