Habari Picha

MAKADA WA CCM WILAYANI ILEMELA WABANWA

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka huu, wametahadharishwa kutotumia pesa (rushwa) kwenye uchaguzi huo.

Hayo  yalibainishwa jana na Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela, Acheni Maulid aliyebainisha kwamba wagombea ambao majina yao yatapitishwa wamuombe Mungu kwani yeye ndiye anayechagua nani  awe kiongozi hata kama watatumia rushwa kama hajapanga  hawawezi kushinda.

Alisema tarehe Agosti 08 hadi 10 mwaka huu kutakua na kikao cha kuwajadili wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na hivyo kuwataka wale ambao majina yao yatapitishwa watambue kwamba ni marufuku kufanya mikutano, mikusanyiko pamoja na kutumia rushwa kwani atakaye bainika ataondolewa kwenye kinyanganyiro hicho.

Alisema jumla ya wanachama 214 walijitokeza kuchukua fomu huku 171 pekee ndio waliofanikiwa kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya wilaya hiyo.

Aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti wilaya kuwa ni  13 ambao ni  Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Nelson Stanley Mesha anayetetea nafasi hiyo, Abubakary Francis Kweyamba, George Massabu Kabambo, Donald Nkwabi Chemo, John Saulo Kafumbi, Mashaka Lucas Biswalo, Abel Katura, Kandawala Julius, Paul Adrian Kitundi, Ruth Mpangalala, Dorah Vedasto Mtengule, Nuru Ramadhani Nsula na Lucia Michael.

Kadhalika alisema jumla ya  makada 15 wamejitokeza kuwania nafasi ya Katibu wa  Siasa na Uenezi wilaya, huku 44 wakijitokeza kuwania nafasi ya Ujumbe halmashauri kuu wilaya.

Bonyeza HAPA kusoma zaidi

Recommended for you