Habari Picha

MAKONDA AWA KIVUTIO KWA VIJANA JIJINI MWANZA.

on

Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoani Mwanza, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kukijenga chama kwa weledi kwani ipo faida kubwa ya kufanya hivyo.

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, aliyasema hayo jana kwenye kikao cha kujitambulisha kwa vijana hao kilichofanyika katika ukumbi wa “Gandh Hall” Jijini Mwanza.

Amiry alikuwa akizungumza na vijana hao ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kujitambulisha katika wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, ambapo jana ziara ya kujitambulisha ilikuwa katika wilaya ya Nyamagana.

“Kwa jinsi ninavyojitolea kufanya kazi, siku moja nitakuja kuwa Makonda (Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa) wa Mwanza hivyo nanyi vijana fanyeni kazi kwa weledi Magufuli (Rais John Magufuli) anawaona”. Alisisitiza Amiry.

Aidha Amiry aliwasihi vijana kufanya kazi kwa kufuata kanuni wakikitetea na kukilinda chama cha Mapinduzi CCM ikiwemo kutangaza mema yote yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Nyamagana, Hussein Kim, alisisitiza kwamba Makonda amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana nchini kutokana na uchapaji wake wa kazi, ndiyo maana amekuwa hamasa kubwa kwa vijana Jijini Mwanza.

Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odilia Bathoromayo, alibainisha kwamba kasi ya vijana kujiunga na Chama cha Mapinduzi imeongezeka katika wilaya yake ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka huu, zaidi ya vijana 1,500 wamejiunga na chama hicho.

Ziara ya Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza katika wilaya ya Nyamagana imegusa ufunguzi wa mashina la UVCCM katika matawi ya Mhandu, Aman Iseng’he B yote katika Kata ya Mhandu pamoja na Shina la Nguvu Kazi kata ya Mbugani na kushuhudia pia uchaguzi wa viongozi wa tawi la Unguja ambapo alisisitiza mashina hayo kutumika kujadili mambo mema ikiwemo uundaji wa vikundi vya miradi ya ujasiriamali kama ufugaji wa kuku.

Pia katibu huyo alikutana na viongozi na wanamichezo kutoka kituo cha michezo cha Marsh Academy na kukuta kituo hicho kikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kodi ya pango na kusafirisha wachezaji wa timu hiyo waliochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ya Wanawake ili kwenda kambini ambapo aliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali mkoani Mwanza ili kutatua sehemu ya changamoto hizo.

Aidha Katibu huyo pia aliwatembelea wanafunzi wenye mtindio wa akili katika shule ya msingi Mbugani ambapo alikutana na waalimu na wazazi wa watoto hao ambapo aliwapongeza waalimu na wazazi wao kwa malezi mema na kuwasihi wazazi wenye watoto wa aina hiyo kutowaficha majumbani.

Vijana wa UVCCM wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry

Wachezaji wa kituo cha michezo cha Marsh Academy wakimsikiliza Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry

Mjumbe wa halmashauri Kuu CCM, Ahmed Misana (kushoto) akisalimiana na Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry (kulia).

Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Nyamagana, Hussein Kim akisalimiana na wachezaji wa kituo cha michezo, Marsh Academy

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akisalimiana na wachezaji wa kituo cha michezo, Marsh Academy

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akisalimiana na wachezaji wa kituo cha michezo, Marsh Academy

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akizungumza na wana CCM kata ya Mbugani

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry,akifungua shina la Aman Isegenghe B kata ya Mhandu

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akisalimiana na balozi mtaa wa Shugunga kata ya Mhandu baada ya kumkabidhi bendera ya CCM

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akizungumza na wana UVCCM kata ya Mhandu

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, pamoja na viongozi wengine walifika nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa Kata ya Mhandu, Lucas Wambura, kutoa salamu za pole kwa mkewe baada ya msiba wa diwani huyo.

Ziara ikiendele wilayani Nyamagana

Mapokezi ya Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry wilayani Nyamagana

Vijana wa UVCCM wilayani Nyamagana

Yonas Alfred ambaye ni DAS Nyamagana, akisalimia kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tarime,

Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Nyamagana, Hussein Kim, akizungumza kwenye kikao cha UVCCM wilayani Nyamagana

Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Nyamagana, Hussein Kim, akizungumza kwenye kikao cha UVCCM wilayani Nyamagana

Zaidi ya vijana 200 walijiunga na CCM na kupokea kadi za chama hicho

Wanachama wapya wa CCM wakipokea kadi za chama hicho kutoka kwa Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry.