Habari Picha

Mfumo wa Malipo kwa Kadi za Benki ya CRDB wapokelewa vyema Mwanza

on

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dr.Chales Kimei amefanya ziara Jijini Mwanza na kukutana na wateja mbalimbali wa benki hiyo ikiwemo taasisi zinazotoa huduma kupitia malipo kwa njia ya kadi za CRDB.

Dr.Kimei aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa benki hiyo ametembelea hospitali ya Kanda ya Ziwa Bugando, hospitali ya Rufaa mkoani Mwanza Sekour Toure, kampuni ya huduma za meli Marne Services pamoja na kampuni ya huduma za usafiriji majini Kamanga Feri.

Katika maeneo aliyopita, Dr.Kimei amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya wateja na benki ya CRDB ambapo ameahidi ushirikiano zaidi ikiwemo huduma za mikopo yenye riba nafuu na kwa haraka zaidi.

Aidha amepongeza matumizi ya malipo kwa njia ya kadi katika taasisi mbalimbali ikiwemo hospitali ya Rufaa Sekour Toure ambapo mfumo huo umeongeza kasi ya ukusanyaji mapato na hivyo kuondoa udanganyifu wa malipo.

Mkurugenzi Mkuu benki ya CRDB Dr.Charles Kimei (katikati), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya hosptali ya Sekour Toure Christopher Gachuma (kulia). Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na hospitali ya Sekour Toure.

Mmoja wa wateja wanaotumia malipo kwa njia ya kadi katika hospitali ya Rufaa Sekour Toure.

Mkurugenzi Mkuu CRDB akizungumza na uongozi wa kampuni ya Marne Services.

Mkurugenzi Mkuu benki ya CRDB (kulia), akizungumza na uongozi wa kampuni ya Kamanga Feri Ltd.

 

Recommended for you