Habari Picha

MAMA MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AITIKIA WITO WA MUNGU

on

Mama Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Mercy Kulola (pichani juu), jana Julai 29,2017 alitunukiwa Diploma yake ya uchungaji baada ya kuhitimu masomo ya biblima katika Chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza ngazi hiyo ya Diploma na sasa ataitwa Mchungaji Mercy Kulola.

Ni baada ya Mama Mchungaji Kulola, bila kushinikizwa na mtu, kuitia wito wa kumtumikia Mungu na kuamua kwenda kusoma ili kuongeza ujuzi zaidi kwa ajili ya kuitenda kazi hiyo. “Namuomba Mungu anisaidie kuitenda kazi yake bila Mawaa”. Anasema Mchungaji Mercy Kulola.

Baada ya mahafali yaliyofanyika viunga vya chuo cha St.Paul, waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, walimuandalia hafla ya kumpongeza iliyofanyika kanisani hapo majira ya jioni.

BMG tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Mchungaji Mercy Kulola kwa hatua hiyo muhimu katika maisha yake.

Tazama picha ilivyokuwa

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola akimpongeza mkewe, Mchungaji Mercy Kulola kwa kuhitimu elimu yake ya uchungaji ngazi ya Diploma, katika Chuo cha Biblia St.Paul Jijini Mwanza

Mchungaji Mercy Kulola (katikati) alihitimu masomo yake ya uchungaji na kutunukiwa ufaulu wa juu katika Chuo cha St.Paul Jijini Mwanza jana Julai 29,2017

Baadhi ya waumini waliohudhuria hafla hiyo

kumbukumbu adhimu

Wazee wa Kanisa na kulia ni mwanafamilia

Mchungaji Mercy Kulola akitoa shukurani zake kwa waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kumuandalia halfa ya kumpongeza baada ya kuhitimu masomo yake ya uchungaji ngazi ya Diploma

Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akitoa salamu zake na kumpongeza mkewe kwa kuitikia sauti ya Mungu na kwenda kusomea uchungaji bila kushinikizwa na mtu yeyote

Zawadi wa Mchungaji Mercy Kulola baada ya kuhitimu masomo yake ya uchungaji

Salamu za pongezi kutoka kwa Katibu wa kwaya ya Havillah

Zawadi

Muda wa zawadi

Muda wa pongezi

Pongezi

Mhitimu Mchungaji Meryc Kulola, akimnywesha shampeni mmewe Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola

Joram Samweli kutoka EAGT Lumala Mpya akifungua shampeni

Mwenyekiti wa kamati ya sherehe akipokea keki

Mchungaji Mercy Kulola akimlisha keki mzee wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya

Muda wa kulishana keki ishara ya upendo

Wasaa wa kukata keki ya pongezi

Mchungaji Dkt.Daniel Kulola na mkewe Mchungaji Mercy Kulola kwenye hafla ya jioni

Ndugu, jamaa na marafiki kwenye picha ya pamoja.

 

Recommended for you