Burudani

Mambo Makubwa kutoka Famara Promotions And Entertainment 2017

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Katika harakati za kuendeleza na kuunga mkono  mziki za injili nchini , Famara Promotions and Entertainment imezindua  tovuti, jarida la mtandaoni pamoja na  TV online, ambavyo vitatumika  kupromoti mziki huo.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi CCM Kirumba jijini hapa kwenye tamasha   la Lakwetu  Concert 2017 Boxing Day Fever na kuzinduliwa na Diwani wa Kata ya Mirongo Hamidu  Said kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire ambaye alipata fursa ya kuzindua  tovuti inayoitwa www.GOSPEL255.com, jarida  ambalo ni GOSPEL255 Magazine Online pamoja na Famara TV Online.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel alisema, huduma zilizozinduliwa zitasaidia kutoa fursa kwa waimbaji,wachungaji na maaskofu kutangaza shughuli zao za injili  mkoani hapa na taifa kwa ujumla.

Fanuel alisema,mbali na huduma hizo pia walizindua albam ya mwimbaji wa nyimbo za injili  Florence Mackenzi  kutoka Zanzibar  iitwayo Ipo Faida sambamba na kuongeza kuwa wanatarajia kuwa na tamasha kama hilo Kahama januari 2018, Morogoro Februari,Mwanza kwa mara nyingine mwezi Machi huku  Aprili itakua Dodoma.

Pia alisema, wameamua kuanzisha huduma hizo baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa watumishi wa Mungu wengi eneo hili wapo nyuma, hivyo wanaamini itakuwa baraka kwa madhehebu yote katika kupeleka mbele gurudumu la injili.

Naye Mgeni Rasmi Hamidu Said alisema,atafikisha yale waliiomba kwa Meya sambamba na kuzungumza namna ya kuandaa mashindano ya kwaya pamoja na kutoa zawadi ili zifanye vizuri na jiji la Mwanza liweze kuunga mkono muziki wa injili.

Said aliipongeza Famara Promotions and Entertainment kwa kuanzisha huduma hizo ambazo zitasaidia waimbaji wa muziki wa injili kujitangaza.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano  Mawasiliano wa Famara Promotions and Entertainment Fortunata Projestus alisema, tamasha hilo limefanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza ilikua mwaka jana,waliguswa kuanzisha baada ya kuona majukwaa ya waimbaji wa nyimbo za injili ni machache, hivyoo wanaamini miaka ijayo litakua kubwa na kutoa fursa na ajira kwa waimbaji wengi wa muziki huo ndani na nje ya nchi.

Projestus alisema, kama taasisi wana malengo ila wanachangamoto ya udhamini kwa ajili ya kufanikisha kuuandaa matamasha kama hayo mijini na vijijini pamoja na uhitaji wa fedha wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali ikiwemo kamera ambavyo vitatumika katika huduma walizozindua ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Hata hivyo Mwiimbaji wa nyimbo za injili Florence Mackenzi  aliyepata fursa ya kuzindua albam yake ya pili yenye nyimbo nane ya Ipo Faida alisema, anamshukuru Mungu kwa kumpa kibali hivyo anaimani kupitia yeye albam hiyo itafanya vizuri.

Mackenzi alisema, kuanzishwa kwa tovuti kwa ajili ya muziki wa injili, jarida la mtandaoni na Tv online itawasaidia waimbaji wa nyimbo hizo kutambulika na kuendelea kutokana na zama hizi za kidigitali kila kitu ni kwanjia ya mtandao hivyo aliwapongeza waanzilishi wa huduma hizo

Recommended for you