Audio & Video

Mambo Muhimu yaliyosisitizwa na TCRA hii leo Jijini Mwanza

on

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kupitia Kamati yake ya Maudhui leo Februari Mosi 2018 imetoa semina kwa Wahariri na Wataarishaji wa vipindi vya Televisheni na Redio kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, iliyofanyika Jijini Mwanza.

Mada mbalimbali zimewasilishwa kwenye warsha hiyo ikiwemo Maudhui ya Kitamaduni iliyowasilishwa na Derrick Murusuri, Maudhui yanayolenga Maendeleo iliyowasilishwa na Joseph Mapunda pamoja na Misingi Bora ya Utangazaji iliyowasilishwa na Abdul Ngarawa.

Mada zote zimelenga kuwahimiza waandaaji wa vipindi kuzingatia sheria na kanuni za utangazaji na hivyo kuandaa vipindi bora vinavyochochea maendeleo ya taifa badala ya kuandaa vipindi vyenye mtazamo hasi katika jamii.

Ungana na BMG Habari #PamojaDaima kujua mambo muhimu yaliyozungumzwa wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.

Viongozi wa Kamati ya Maudhui TCRA

Uwasilishaji wa mada kwenye warsha hiyo.

Recommended for you