Audio & Video

MANENO YA RAIS KENYATTA WA KENYA BAADA YA USHINDI

on

BMG Habari, Pamoja Daima

Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza mgombea urais wa Chama cha Jubilee, Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa taifa hilo kufuatia uchaguzi uliofanyika jumanne wiki hii, Agosti 08,2017. Makamu wa Rais atakuwa William Ruto.

Kenyatta ametangwa majira ya saa nne usiku leo ijumaa, Agosti 11,2017 kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo baada ya kupata kura 8, 203, 290 sawa na asilimia 54.27 na hivyo kumshinda mgombea wa muungano wa NASA, Raila Odinga aliyepata kura 6, 762,224 sawa na asilimia 44.74.

Rais Kenya ambaye ametetea muhura wake wa pili wa uongozi, amewashukuru wakenya na kuwasihi kuendelea kuwa wamoja kwa kusema uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo hivyo waendelee kudumisha amani yao. Pia ameishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri.

Ameahidi kushirikiana na viongozi wengine wa upinzani bila ubaguzi akisema wao si maadui bali ni raia wa nchi moja hivyo wanafaa kuungana pamoja na kwamba hakuna haja ya kuwepo fujo kwani wanasiasa huja na kuondoka. Amesema wakenya wote ni washindi na hakuna aliyeshindwa kwenye uchaguzi huo hivyo waungane pamoja kuijenga nchi yao.

Shamra shamra zimeendelea kurindima katika viunga mbalimbali nchini Kenya licha ya hapo awali baada ya uchaguzi kuripotia visa vya hapa na pale vya uvunjifu wa amani ambavyo vilikuwa vikifanywa na baadhi ya wafuasi wa wagombea na kuwalazimu polisi kupambana nao.

Kabla ya matokeo rasmi kutangazwa, upinzani ulikuwa ukilalamikia matokeo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa kwa kusema kwamba kura zilivurugwa baada ya mitambo ya IEBC kudukuliwa

Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ambaye amekiri kwamba licha ya changamoto kadhaa kukumba mfumo mpya wa kutangazia matokeo, lakini tume hiyo ilifanikiwa kutangaza matokeo hayo bila tatizo.

Waliojiandikisha kupiga kura nchini Kenya walikuwa 19,611,423 na waliopiga kura ni 15,073,662 sawa na asilimia 78.91 huku kukiwa na wingi wa kura zilizoharibika ambazo takribani 399 ,935.

Video imerekodiwa CitizenTv Kenya

 

 

Recommended for you