Audio & Video

Viongozi wazungumzia manufaa ya bandari za Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Huduma ya usafirishaji wa mabehewa ya mizigo kwa kwa njia meli kupitia Ziwa Victoria kutoka bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda), imezinduliwa hii leo katika bandari ya Mwanza Kusini.

Hatua hii inajiri ikiwa ni mara ya kwanza tangu huduma hiyo isitishwe miaka 10 iliyopita ambapo mabehewa matano ya mizigo yaliyosafirishwa kwa njia ya treni kutoka mkoani Morogoro yamefaulishwa kuingia kwenye meli ya MV.Umoja kuelekea kwenye bandari ya Portbell nchini Uganda.

Viongozi kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamezungumzia juhudi zilizofanyika kurejesha huduma hiyo pamoja na manufaa yanayotarajiwa kupatikana.

SOMA Uzinduzi wa huduma katika bandari ya Mwanza Kusini hadi Portbell Uganda

Recommended for you