Habari Picha

ITUMIE TOVUTI YA BMG KWENYE MAONESHO YA NANE NANE 2017

on

Maonesho ya wakulima na wafugaji Nane Nane 2017 yameanza katika Kanda mbalimbali nchini ikiwemo Kanda ya Ziwa ambapo yanafanyika katika uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza huku kitaifa yakifanyika katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.

Lengo ni kuwawezesha wakulima na wafugaji kuonesha mazao na bidhaa zitokanazo na mazao yao huku pia makampuni mbalimbali ikiwemo yanayotengeneza na kuuza zana za kilimo na biashara yakitumia fursa hiyo kunadi bidhaa zake.

Tovuti ya www.bmghabari.com inawakaribisha watu wote ikiwemo halmashauri, wajasiriamali na wamiliki wa makampuni mbalimbali kutangaza shughuli zao katika msimu huu wa Maonesho ya Nane Nane ambayo yalianza tangu Agost Mosi hadi Agost 08,2017.

Kumbuka kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni “Zalisha kwa tija mazao ya bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

Wasiliana na BMG kupitia nambari 0757 43 26 94. BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you