Audio & Video

Hakika hii ni Tanzania Mpya

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine baada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

Rais Dk.John Magufuli amewaongoza viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na watanzania kupokea ndege mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262 aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imetua katika ardhi ya Tanzania hii leo majira ya saa 11.25 jioni.

Ndege hiyo kabla ya kutua ilichukua dakika kadhaa ikionekana katika anga la Tanzania huku Rais Magufuli  na watanzania kwa ujumla wakiishangilia wakati inashuka.

Mbali na Rais Magufuli pia alikuwepo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Rais Magufuli amesema kuwa ujio ndege ni heshima na ni mali ya Watanzania na kuwataka wananchi watangulize maslahi ya Tanzania na kwamba tabia ya wizi, dhuluma haina nafasi na wengi.

“Tumeona mkono wa Serikali uingie ili kila kinachoingia tukione.Watanzania wengi wanaunga mkono na wale wachache ambao hawaungi mkono Mungu atawaumbua,”amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege hiyo amesema ni fahari kubwa kwani ni mali ya Watanzania. Amesema wakati Rais anahimiza watu kubana matumizi wengi walikuwa hawamuelewi lakini sasa wanaona yanayofanyika.

Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ndani ya ndege hiyo amesema Rais anayo nia ya dhati ya kuleta maendeleo na kwamba kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu imesababisha ujio wa ndege hiyo.

“Rais anahimiza watu kufanya kazi na matoke yake watu wanafanya kazi na kulipa kodi ambayo ndio imesababisha kununulwa kwa ndege hii na nyingine,”amesema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua katika ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani

Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikipewa heshma ya kumwagiwa maji (Water Salute ) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu

Video na MAELEZO TV

Recommended for you