Audio & Video

Ni noma mapokezi ya Waziri Jaffo katika shule ya wasichana Ngaza

on

George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe.Suleiman Jaffo amefurahishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali Jijini Mwanza.

Waziri Jaffo ameyasema hayo hii leo Mei 13, 2018 alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu.

Akiwasili katika shule ya wasichana Nganza kukagua miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa mabweni ya wasichana, Waziri Jaffo amepata mapokezi makubwa na ya kusisimua.

Waziri Jaffo amekagua miradi mbalimbali Jijini Mwanza ikiwemo eneo la ujenzi wa stendi ya malori Buhongwa, eneo la ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi, mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana Butimba, barabara ya Mulungushi, machinjio ya kisasa Igoma pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Nyashana na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Waziri Suleiman Jaffo (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella. 

Waziri Jaffo akipokea taarifa ya ujenzi kutoka kwa Mkuu wa shule ya sekondari Nganza, Mwl. Yasinta Lyimo. 

Waziri Jaffo akiwakiwa na waalimu washule ya wasichana Nganza.

Waziri Jaffo akilakiwa na waalimu shule ya sekondari ya wasichana Nganza. 

Waziri Jaffo akizungumza alipotembelea shule ya wasichana Nganza.

Waziri Jaffo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia).

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mhe.Marry Tesha akiwasilisha salamu zake wakati wa ziara hiyo.

Mkuu wa shule ya wasichana Nganza, Mwl.Yasinta Lyimo akisoma taarifa ya ujenzi wa mabweni na miradi mingine shuleni hapo.

Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya wasichana Nganza, Christopher Mwita Gachuma akitoa salamu zake wakati wa ziara hiyo ambapo ameungana na wanafunzi wa shule hiyo kumuomba waziri Jaffo kusaidia uoatikanaji wa gari la shuleni hapo.

Mwanafunzi Rachel Mkenda akitoa salamu za shukurani kwa Waziri Jaffo kwa niaba ya wanafunzi wenzake ambapo wamemuomba kuwasaidia upatikanaji wa gari la shule ili kuwaondolea adha ya kukosa usafiri hususasi inapotokea dharura ya mwanafunzi kuugua usiku.

Baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari Nganza ambayo ina wanafunzi hadi kidato cha sita. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI aanza ziara ya kikazi Jijini Mwanza

Recommended for you