Habari Picha

Mapokezi ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Jijini Mwanza

on

Waziri Mkuu Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Taifa, Mhe.Mizengo Peter Kayanza Pinda amepokelewa hii leo Juni 02, 2018 Jijini Mwanza, akiwa safarini kuendelea mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya kichama.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 

Mhe.Pinda aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa chama, amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa moja na dakika kadhaa asubuhi na kulakiwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella, Mkuu wa Mkoa Mara Mhe.Adam Malima pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Taifa, Mhe.Mizengo Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mara Mhe.Adam Malima (kulia).

Mhe.Pinda akisalimiana na Christopher Mwita Gachuma ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Mhe.Pinda akisalimiana na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza.

Mhe.Pinda akisalimiana na Kaimu OCD wilayani Ilemela.

Pia Mhe.Pinda amefanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia).

Wiki iliyopita Rais Magufuli aliwateua Mhe.Pinda (kulia) pamoja na Makongoro Nyerere (kushoto) kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi CCM, Makongoro Nyerere (kushoto).

Pia Mhe.Pinda ameambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Mama Gaudensia Kabaka (wa pili kushoto).

Mhe.Pinda amepata mapumziko mafupi Malaika Hotel Jijini Mwanza kabla ya kuelekea mkoani Mara.

Recommended for you