Burudani

Masanja atamba kufanya kweli Jijini Mwanza

on

Judith Ferdinand, BMG

Mchekeshaji na mwimbaji wa nyimbo za njili hapa nchini, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amewataka wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa albamu ya “Tuliza Mawimbi” iliyoandaliwa na kwaya ya Ebenezer Family Band.

Amesema katika uzinduzi huo utakaofanyika leo September 09, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba, atatumbuiza nyimbo zake mbalimbali ikiwemo wimbo wake mpya uitwao Kemea Pepo.

“Naomba wakazi wa Mwanza wafike bila kukosa iwe kwa usafiri wa gari, baiskeli, bajaji hata kwa miguu ili washuhudie uzinduzi huo na kumsifu Mungu kupitia injili”. Amesema Masanja.

Uzinduzi huo pia utahudhuriwa na kwaya mbalimbali ikiwemo AIC Makongoro, Revival Mission Band na Emaus Band ambapo kiingilio ni shilingi 2,000 kwa watu wazima na shilingi elfu 1,000 kwa watoto.

Recommended for you