Habari Picha

MASHAHIDI WA YEHOVA WAKUTANA JIJINI MWANZA

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Watanzania wametakiwa kuachana na vitendo vya uovu bali wadumishe amani na upendo uliopo kwa kuishi maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu ikiwemo kujijengea desturi ya kusoma biblia na kumtumikia Mungu.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mhubiri wa Habari Njema wa Mashahidi wa Yehova, Livingstone Mosha katika kusanyiko la siku tatu linalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mosha alisema kusanyiko hilo limeandaliwa na Mashahidi wa Yehova kwa lengo la kufundisha jamii bila kubagua dini, kusoma na kujua biblia ambapo limejumuisha washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Geita na Mara.

“Nyakati za kisasa Mashahidi wa Yehova tupo kwa ajili ya kufundisha jamii kuhusu biblia, hivyo kusanyiko  hili la siku tatu linawataka watu wasife moyo, wamtii na kumtumikia Mungu ili kupata baraka na kuacha kufanya maovu wasije pata hasara”. Alisema Mosha.

Alisema vijana watapata mafunzo kupitia biblia na watakua karibu na Mungu, jambo litakalosaidia kuwafanya wawe na maadili na kuacha kufanya vitendo viovu visivyopendeza kwa jamii.

Aidha aliwahimiza wanajamii wanapopatwa na maradhi wakimbilie hospitalini huku wakimuomba Mungu kwani ndiye mwenye uwezo wa kuponya.

Recommended for you