Audio & Video

Kocha Mbao FC aumizwa na sare ya nyumbani dhidi ya Maji Maji FC

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Timu ya soka ya Mbao FC ya Jijini Mwanza imelazimishwa sare ya bao 2-2 dhidi ya Maji Maji FC ya mkoani Ruvuma katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba hii leo.

Mbao walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa mchezaji Boniphace Maganga dakika ya 60 ambaye pia aliongeza bao la pili dakika ya 62.

Hata hivyo Maji Maji walitoka nyuma na kusawazisha magoli hayo kupitia kwa Marcel Boniventure aliyefunga bao la kwanza dakika ya 81 na bao la pili ndani ya dakika tatu za nyongeza.

Kwa matokeo hayo Mbao wamefikisha pointi 24 huku Maji Maji wakifikisha pointi 20 ambapo timu zote zinapambana kuhakikisha zinabaki ligi kuu.

Recommended for you