Audio & Video

Mbunge jimbo la Bukombe mkoani Geita awatoa hofu wananchi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mbunge Jimbo la Bukombe mkoani Geita Doto Biteko (CCM) amewatoa hofu wananchi wa jimbo hilo kuhusu upatikanaji wa huduma ya umeme na kubainisha kwamba Vijiji 76 vinatarajia kunufaika na umeme wa REA.

Biteko ametoa kauli hiyo jana Julai 30, 2018 wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi Ushirombo.

Amesema kuna zaidi ya transfoma 150 ambazo zitafungwa wilayani Bukombe na hivyo kusaidia wananchi wa maeneo mengi kupata huduma hiyo na hivyo kuwahimiza kuwa wavumilivu wakati utekelezaji unaendelea.
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Katibu wa Siasa na Uenezi mkoani Geita, David Azaria (kushoto) akitoa salamu zake kwenye mkutano huo
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Bukombe, Doto Biteko
Taswira ya mkutano huo uliofanyika uwanja wa stendi Ushirombo

Recommended for you