Audio & Video

Mbunge Nyamagana afunga Mafunzo ya zao la Muhogo mkoani Mwanza

on

Afisa Kilimo mkoani Mwanza, Innocent Keya akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

Mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza Stanslaus Mabula, leo amefunga mafunzo kuhusu zao la kilimo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo kwa takribani washiriki 100 mkoani Mwanza.

Mafunzo hayo yaliyoanza juzi februari 08,2018 katika ukumbi wa New Mwanza Hotel, yalilenga kuhamasisha ulimaji na uongezaji thamani katika zao la muhogo kutoka kuwa zao la chakula hadi zao la biashara.

Mratibu wa Mafunzo hayo Denis Lekela Nyamlekela Kankono ambaye pia ni Katibu wa Siasa na Uenezi (CCM) wilayani Ilemela, amebainisha kwamba mada mbalimbali ikiwemo muhimu wa zao la muhogo na fursa zake, uzalishaji, utuzaji wa shamba na changamoto zake, aina za mbegu na muda wa kukomaa, mchakato wa uvunaji na uhifadhi, usindikaji, usajili wa leseni za biashara pamoja na masoko ya muhogo zimefundishwa kwenye mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yalishirikisha washiriki kutoka wilaya za Nyamagana, Ilemela, Misungwi na Ukerewe ambapo washiriki hao wamemuomba mbunge Mabula kuwasaidia kupaza sauti ili kupitia kikundi watakachokiunda, waweze kukopesheka kupitia taasisi za kifedha ili wapate mikopo itakayowasaidia kuanzisha na kuendesha shughuli za kilimo ikiwemo zao la muhogo.

Mwanaidi Kiya ambaye ni Mtaalamu wa Hifadhi ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti Habari Leo/ Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula.

Recommended for you