Audio & Video

Salamu za pongezi kutoka kwa Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana

on

Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Ahmed Misanga (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Makondakta wa Daladala Mkoa wa Mwanza MWAREDDA, Mjalifu Manyasi (kushoto).

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nyamagana imetoa pongezi kwa madereva wa daladala na makondakta mkoani Mwanza kwa kujiunga na bima ya afya NHIF kupitia umoja wao wa MWAREDDA.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Ahmed Misanga aliyemwakilisha Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Stanslaus Mabula kwenye hafla ya kukabidhi kadi za NHIF kwa madereva na makondakta 36 ambao ni wanachama wa MWAREDDA.

Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana akisalimiana na madereva daladala na makondakta mkoani Mwanza

Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana akisalimiana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha (kushoto)

Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha akisalimiana na baadhi ya madereva na makondakta mkoani Mwanza

Tazama BMG Online TV hapa chini

Pia SOMA Nyamagana akabidhi Bima za NHIF kwa madereva na Makondakta

Recommended for you