Audio & Video

Mbunge Neema Mgaya asaidia uboreshaji huduma za afya mkoani Njombe

on

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Njombe, Neema Mgaya amekabidhi mifuko ya saruji tani tatu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya mbalimbali wilayani Ludewa.

Pia ametembelea hospitali ya wilaya Ludewa na kukabidhi mashuka kwa ajili ya wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali za upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wilayani humo.

Aidha amekabidhi mashuka katika Zahanati na Vituo vya Afya vipatavyo 13 mkoani Njombe pamoja na mifuko ya saruji zaidi ya tani 10 lengo likiwa ni kusaidia ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati ikiwemo Kituo cha Afya Lugawala, Ludewa K pamoja na Zahanati ya Gereza la Ndulamo Makete.

Pia amekabidhi mashuka takribani 400 katika Zahanati na Vituo vya Afya katika wilaya za Ludewa, Makete, Wanging’ombe na Njombe mkoani Njombe pamoja na Hospitali za wilaya Makete, Ludewa na Njombe ambapo vitu vyote, mifuko ya saruji na mashuka vina thamani ya shilingi saba.

Recommended for you