Audio & Video

Zaidi ya shilingi bilioni mbili kumaliza kero ya maji Bukombe

on

Na George Binagi, Bukombe

Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Mashaka Biteko (CCM) amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika jimbo hilo.

Biteko aliyasema hayo Agosti 02, 2018 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya hadhara jimboni Bukombe, iliyolenga kuwaeleza utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati akiomba kura.

Aidha Biteko alisema serikali inaunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo ikiwemo ujenzi wa Zahanati kila Kijiji na Kata katika jimbo hilo.

Katika sekta ya elimu, Biteko aliunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Kabulima Kata ya Uyovu kwa kuwachangia mifuko 100 ya theluji kwa ajili ya ujenzi wa madarada ya shule ya kijiji hicho.

Hata hivyo katika mkutano huo, wananchi walimuomba mbunge Biteko kuwasaidia ili waunganishiwe huduma ya umeme kupitia mradi wa REA III awamu ya kwanza, kwani wengi wao wamekuwa wakiomba kupata huduma hiyo bila mafanikio.

Mbunge jimbo la Bukombe, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kabulima, Kata ya Uyovu

Wakazi wa Kata ya Uyovu wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Bukombe, Doto Biteko

Wakazi wa Kata ya Uyovu wakiuliza maswali kwa mbunge Doto Biteko

Kwenye mkutano huo, takribani wanachama 10 wa Chadema walijiunga na CCM

Recommended for you