Audio & Video

Benki ya NMB yasaidia kutatua changamoto za afya na elimu Jijini Mwanza

on

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza jana wakati wa zoezi la kupokea madawati yaliyotolewa katika shule ya msingi Mwenye pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa katika Zahanati ya Pasiansi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Benki ya NMB imeahidi kushiriki na serikali katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kijamii hususani katika sekta ya elimu na afya.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Ziwa, Abraham Austino aliyasema hayo jana Mei 14, 2018 wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 60 katika shule ya msingi Mwenge pamoja na vifaa tiba katika Zahanati ya Pasianzi, zote katika Manispaa ya Ilemela.

Alisema kwa mwaka huu benki hiyo imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ushiriki wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Akipokea vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni kumi vilivyotolewa na benki ya NMB, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella aliipongeza benki hiyo kwa utayari wake katika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii na kuwa benki inayoongoza kwa kutoa gawio kubwa kwa serikali.

Uongozi wa shule ya msingi Mwenge uliiomba benki ya NMB kuendelea kusaidia changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Magu ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemelea mkoani Mwanza, Mhe.Khadija Nyembo akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo ambapo aliishukuru benki ya NMB kwa mchango wake katika kutatua changamoto za elimu na afya katika jamii.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisema kwa mwaka huu benki hiyo imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.

Meneja wa benki ya NMB tawi la Rock City, Jackline Timoth ambapo alisema benki hiyo itaendelea katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto), akipeana mkono na Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa Abraham Augustino (kulia), wakati akipokea madawati 60 yenye thamani ya shilingi milioni tano, yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shule ya msingi Mwenge Manispaa ya Ilemela.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto), akisalimiana na Meneja wa benki ya NMB tawi la Rock City, Jackline Timoth wakati wa hafla hiyo.

Katika hafla hiyo, uongozi wa shule ya msingi Mwenge ulitoa cheti cha shukurani kwa benki ya NMB.

Madawati haya yatasaidia kuondoa changamoto ya madawati shuleni Mwenge.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mwenge wakiimba shairi wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya vitanda vilivyotewa na benki ya NMB katika Zahanati ya Pasiansi Manispaa ya Ilemela.

ISOME PIA HABARI HII Mawakala wa benki ya CRDB watakiwa kuendeleza uadilifu

Recommended for you